April 22, 2012

MAREHEMU STEVEN KANUMBA ALIKUWA FREEMASON?GAZETI LA NYAKATI LIMEANDIKA

Ramsey Kassim | 5:44:00 PM | |
Nilipoandika wiki inayoisha leo juu ya imani na ujinga juu ya Freemason hakika kumbe sikujua ukubwa wa tatizo.nimepokea simu nyingi na meseji zaidi ya 200 kati ya hizo wengi wakionekana kusema mimi ndiye mjinga ninayepingana na ukweli kuwa Freemason hawapo.Lakini mimi sikusema hawapo,ila nilisema tunachosema kuwahusu ndiyo ujinga kwani tunawasingizia na kujitia hofu juu ya ujinga wetu wenyewe kutokuwa na imani na kutopenda kusoma wala kijifunza ila kuishi kwa majungu,uzandiki na unafiki wa hali ya juu huku tukijifanya ni waumini wa dini.
Leo gazeti linalojiita la kikristo linachapisha habari tena ukurasa wa mbele juu ya Kanumba kuwa freemason.nimezoea kuona mambo hayo kwenye magazeti ya udaku.kwa hiyo kwangu mimi hili nalo ni gazeti la udaku.sina ugomvi na kanumba kuwa mwanachama wa freemason(kama alikuwa kweli,kwani ni haki yake kujiunga na kundi lolote lisilovunja katiba na sheria za nchi),Lakini gazeti la kikristo lilipaswa kujua ujinga ulioenezwa hata na baadhi ya madhehebu ya kikristo juu ya Freemasons tena dhidi ya ukristo na kujua athari ya habari ya kijinga kama hii kuwa katika gazeti la kikristo,mathalani Nyakati hawaonyeshi kadi ya uanachama wa kanumba kwenye chama hiki,wala halisemi alianza mafunzo kwenye lodge ipi wala ni lini na wapi alijitambulisha kama freemason.Nimeshasema na nirudia tena ni UJINGA kukusanya michoro kwenye nguo ya mtu au mapambo anayovaa kama lilivyofanya Nyakati eti ndiyo ushahidi kuwa mtu fulani ni Freemason.mimi nimeona kwa macho yangu mwenyewe wachungaji wengi wakati wa mahubiri tena wakiwa mimbari wakijishika tumboni wakati wanaongea.naam nimewaona akina mwakasege,mzee wa upako,gwajima,lwakatare,nimewaona akina askofu kulola,kakobe,askofu pengo,malasusa,mokiwa,nimewaona waandishi wa habari,wahadhiri,nimewaona wazazi wangu,naam hata mimi hujishika tumboni ninapoongea.kwa mujibu wa Gazeti la kikristo la Nyakati sisi wote ni Freemason,jamani huu ni UPUMBAVU Fullstop.
Hebu niongeze:yeyote ajitazame vizuri,kama umevaa chupi,kama ukivaa suruali unavaa na mkanda,kama unavaa pete ya ndoa au ya urembo,bangili,kama unanunua bidhaa supermarket,kama unamiliki gari,baiskeli,kama unatibiwa kwenye hospitali kubwa,unasali makanisani,misikitini(kote huko freemason wametawala),kama unavaa tai,koti,viatu,wewe ni freemason tuuu.Naendelea jitazame unapotembea unaanza kwa kutumia mguu wa kulia,unajisaidia haja kubwa kwa kuchuchumaa au kukaa,haya ukipiga muayo unafunika kinywa kwa kitambaa ni freemason wewe,unaweka hela kwenye waleti au pochi,unakunywa soda za koka,maji ya kilimanjaro wewe tayari ni freemason,naam mwanamke umeolewa na unalala ukutani (freemason hawalali karibu na ukuta),haya twende unatumia kipaza sauti kuongea(vifaa vya freemason),unakula nyama ayayayayaya! ndo freemason mkubwa.Jamani hebu tuache UJINGA HUU.
Hivi sisi waafrika tunajidhalilisha? wakoloni walipotuita nyani kasoro mkia haikutosha? tulipoitwa chimpanzee haikutosha? sasa mbona tunatiana hofu zisizo na kichwa wala miguu?eti freemason hawaamini mungu? nani kasema? eti wanauwa watu kwa nguvu za giza! jamani kweli sisi mbumbumbu mzungu wa reli.
zamani tuliwasingizia wazungu kwa udhalili wetu,lakini leo tunaouhuru angalau wa bendera,wengine tumehesabu madirisha ya shule hadi vyuo vya nje,lakini bado tunazungumza ujinga,kwa nini wazungu hawana huu ujinga?sisi mbona tunajidumaza wenyewe? kwa nini tunaunga mkono kwa vitendo tuhuma kwamba sisi tumelaaniwa?
Nimalizie kwa namna ya mwaliko kwa makanisa kwani naona kuna hitaji maalum kufanya hivyo.Huko nyuma ukristo umewahi kuitwa Bangi( An opium of the people),Ni hivi ili kuzuia usanii,shughuli za uongo na mwenendo wa hovyo katika kukabiliana na matatizo ya watu wa siku hizi tunahitaji wachungaji,maaskofu,na wahubiri wasomi walosjifunza wakafunzika elimu mbalimbali ili wafundishe kwa utulivu wakitumia vichwa badala ya matumbo kama wengi wanavyofanya sasa,eti mtu akiweweseka kidogo wanakimbilia kusema eti ni mashetani,mara majini,mara laana za mizimu hivyo anahitaji kuombewa na kadhalika,huku ni kufanya mambo ya kienyeji kuliko hata wapiga ramli.Hali holela kama hii inatia aibu na kinyaa kanisa letu la kristo na inaunga mkono kwamba ukristo ni bangi,wakati kanisa tangu mwanzo lilikuwa kiongozi kwenye elimu ya kisasa.
Basi tunawahitaji viongozi wa dini wasomi watakaoweza kubaini kwa uhakika ugonjwa upi ni ugonjwa wa kimwili,upi wa kisaikosomatiki na upi ni wa kupagawa na shetani kweli.Wachungaji wa hivyowasomi wa kweli watatuepushia kiu holela ya utendaji miujiza na hivyo kutuepusha na aibu mbaya ya kuonekana wasanii na matapeli wa imani.si vyema kanisa kujihusisha na uwongo utakaomtukanisha roho mtakatifu
Jamani kama hamniungi mkono katika hili,basi peke yangu nitabaki maana sitaki kuona mtu anadanganya kama walivyofanya gazeti la nyakati nami nikaa kimya.Msidhani nimehama mada,hapana naongelea UJINGA wa hofu wa freemasons na wahusika wakuu wa kusambaza hofu hiyo ni wahubiri uchwara wanaowatia watu hofu na sasa gazeti la kikristo linaunga mkono ushirikina.si mmesikia injili za siku hizi zinavyohubiri mafanikio na kwamba mkristo hapaswi kuteseka hata kidogo? huu nao ni upotofu na danganya toto,habari za mtu kufufua misukule,habari za kuponya wagonjwa holela kwa miujiza,na ujinga mwingine,ndivyo vinavyokoleza hata huu juu ya freemason,SHETANI anaonyeshwa kuwa na nguvu juu ya Mungu,badala ya kuhubiri shetani na woga hubirini juu ya nguvu ya neema na ushindi wa mkristo na kristo dhidi ya shetani.
Gazeti la nyakati limetia aibu ya milenia.
LUDOVICK
0715 927100: 0753 927100

5 COMMENTS:

Anonymous said...

Tatizo Watanzania bado tu wajinga.. ukimuuliza mtu nini maana ya Free mason ata ajui.. Hajui ata kanuni zake.. ajui wanajiungaje na huo Ufree mason.. kama hamna uhakika mkae kimya.. mnaboa kha!! Afu mnaongea mkiwa hata hamjalewa.. wazima je mngekunywa kidogo haaa aibu

Anonymous said...

Nani amekudanganya freemasons wanatutia hofu ndani yetu wakristo. Mtu hujulikana alivyo kwa matendo yake so kama hilo gazeti la nyakati limefuatilia mienendo ya Kanumba na kuiona ina relate na imani za freemasons hiyo ni opinion yao na wana sababu ya kuandika hivyo. Angalia usije fikiri upo sawa kumbe ni chaka full! Hamna mkiristo aliyesimama katika imani yake anaogopa freemasons bali tunatambua uwepo wao katika jamii na jinsi imani zao zilivyo kinyume na imani za kikirsto.

Anonymous said...

kwanini freemason wahusishwe na kuupinga ukristo kwani shetani yupo kwa ajili ya kuwaangamiza wanadamu walio-wakristo pekee?huu ni ujinga tena usio na kipimo. Kama unaimani basi simamia kwenye imani yako na usishiriki ujinga maana wajinga hujiangamiza kwa ujinga wao wenyewe.

Anonymous said...

ndugu yangu ludovick natumaini kabisa kuwa wewe ni msomi, sasa unatakiwa unapoandika habari kwenye media kama hii jaribu kuwa kwenye point moja husika, ili uwezekufikisha jumbe ulio kusudia . kwenye habari yako umeanza kuongelea kuhusu gazeti la nyakati na kuandika habari za kanumba, na mwishoni ukachanganya wa kristo wote na watanzania wote. kumbuka lililo andika habari hizi ni gazeti na sidhani kama gazeti hili moja lingeweza kukufanya wewe uchanganye watanzania wote katika habari hii na kutumia mameno makali. najuwa wewe ni mwandishi mzuri ila jirekebishe kwa hili utakuwa mzuri zaidi.

Anonymous said...

Mi hasa sijamwelewa aliyeleta mada, kwani yeye hasa shida yake nini? Ana tatizo na wakristo wa tz au anataka kuwaeleza umma kwamba freemansory hawapo na ni dhana ya kufikirika au kuna ujumbe mwingine umeshindwa kuufikisha kwani umegusia waalimu, wainjilisti, wachungaji, maaskofu na pia umegusia uponyaji/miujiza km ni hivyo atafute njia nyingine ya kuelezea kile anachokifikiri au alichokifanyia utafiti kwani ni haki yake. be specific

iam_ramsey © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster